KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Charles Msonde jana Julai 11, 2019 mjini Unguja Zanzibar alitangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019 na kusema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.
Miongoni mwa shule zilizofanya vizuri sana ni pamoja na shule za Feza Boys na Feza Girls, ambazo wanafunzi kutoka shule hizo wameingia kwenye kumi bora ya wanafunzi waliofanya vizuri nchini.
Global TV imefika mpaka shule ya Feza na kuzungumza na baadhi ya wanafunzi hao pamoja na uongozi wa shule.
Comments are closed.