The House of Favourite Newspapers

Walimu 1135 Wapandishwa Madaraja

0

WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Ummy Mwalimu, amesema tayari wameshawapandisha madaraja walimu 1135 kwa halmashauri ya Mwanza kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mei mosi alipokuwa Mwanza.

 

Ummy amesema hayo katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, inayoendelea Jijini Mwanza leo, Juni 14, 2021 ambapo amesema Rais  Samia ni mtu anayetekeleza yale yote anayoyaahidi kwa wananchi wake.

 

“ Rais alikuwa hapa tarehe 1/5/2021 akatuelekeza tupandishe madaraja walimu wote wa msingi na sekondari tumetekeleza ahadi yako walimu wote waliostahili kupanda madaraja katika halmashauri ya Mwanza 1135 wamepandishwa madaraja maana yake kuna utulivu katika shule zetu, watoto watasoma bila shida,” amesema Waziri Ummy.

 

Pia, Ummy amesema katika kuhakikisha elimu inazidi kukua tayari kuanzia mwezi Machi 2021 Rais ameshatoa shilingi bilioni 3.9 kwa ajaili ya kuboresha elimu katika mkoa wa Mwanza huku TAMISEMI ikiwa imeleta shilingi milioni 500 kwa ajili ya hospitali ya Nyamagana.

 

Leave A Reply