Sektretarieti ya ajira imetangaza majina 122 kuingia katika ajira mpya serikalini Februari Mosi 2025.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililochapishwa katika tovuti ya sektretarieti ya ajira, 95 ni walimu wa kada mbalimbali, ambayo ni sawa na asilimia 77.8 ya walioitwa kazini.
Walimu hao wamepangiwa katika halmashauri tatu kama ifuatavyo; Halmashauri ya Manispaa Temeke , Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Manispaa Kinondoni.
Upande wa kada zao, walimu hao wapya walioajiriwa ni kama ifuatavyo: Mwalimu daraja la III B fizikia (14), mwalimu daraja la III B – hisabati (27), mwalimu daraja la III B biashara (4), mwalimu daraja la III C fizikia (8), mwalimu daraja la III C hisabati (28).
Kada nyingine ni: Mwalimu daraja la III C sanaa (2) na mwalimu daraja la III C biashara (12).
Waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili na baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta.