The House of Favourite Newspapers

Walimu 4 wa Chuo kikuu cha Marekani Wadungwa kisu Kwenye Bustani

0

 

WALIMU wanne wa chuo kikuu nchini Marekani wamelazwa hospitalini baada ya kudungwa kisu na mtu asiyejulikana katika bustani ya umma nchini China.

Wakufunzi wa Chuo cha Iowa Cornell walijeruhiwa katika tukio baya wakati wa ziara ya mchana katika bustani hiyo katika mkoa wa Jilin, kaskazini mwa China, taarifa ya chuo ilisema.

Mwakilishi wa Iowa Adam Zabner alisema kaka yake David ni mmoja wa watu wanne waliojeruhiwa katika tukio hilo ambalo alilitaja kuwa la kuchomwa visu.

Alisema kundi hilo lilikuwa limezuru hekalu la eneo hilo siku ya Jumatatu waliposhambuliwa na mwanamume mmoja kwa kisu Zabner alisema kakake alikuwa amedungwa kisu kwenye mkono katika bustani ya Beishan na alikuwa akiendelea kupata nafuu hospitalini.

“Bado hajaachiliwa asubuhi hii lakini anaendelea vizuri,” aliiambia CBS News.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani alisema wanafahamu kuhusu tukio la kudungwa kisu huko Jilin, lakini hakuweza kutoa taarifa zaidi.

Chuo cha Cornell kilisema wakufunzi hao wanne wamekuwa wakifundisha “kama sehemu ya ushirikiano na chuo kikuu nchini China”. Kundi hilo lilikuwa limeandamana na mwanachama wa Chuo Kikuu cha Beihua wakati wa ziara yao katika bustani hiyo Jumatatu.

Mamlaka za Uchina bado hazijajibu juu ya tukio hilo, licha ya picha za tukio hilo kusambazwa haraka kwenye mitandao ya kijamii.Picha zinazozunguka zinaonekana kuonyesha watu wasiopungua watatu wakivuja damu wakiwa wamelala chini.

Hata hivyo tukio hilo linaonekana kufichwa haraka kwenye mtandao wa China.Siku ya Jumanne, utafutaji wa maneno kama vile “wageni Jilin” haukuzaa matunda licha ya kuwa neno la utafutaji linalovuma kwenye mtandao wa Weibo.

Watumiaji wa mtandao badala yake waliingia kwenye mijadala chini ya mada zilizo karibu huku wengine pia wakionekana kuuliza habari zaidi kuhusu tukio hilo.

Pia kuna ripoti chache kuhusu tukio hilo katika vyombo vya habari vya serikali ya China.

KIMEUMANA! WADHULUMIANA OMAN NUSU WAZICHAPE/UKOO WAVURUGIKA-DADA AOMBA MSAADA ARUDI NYUMBANI

Leave A Reply