The House of Favourite Newspapers

Walimu Dar kusafiri bure – DC Makonda

0

1

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

2-001

Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabrouk akifafanua jambo.

3

Mwenyekiti wa Uwadar, William Masanja akizungumza na waandishi wa habari.

4

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva nchini (Tadu), Shaban Mdemu akichangia hoja mbalimbali.

5

Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mapema leo hii ametangaza kuwa walimu wa shule za serikali zilizopo jijini Dar watasafiri bila kulipa nauli kwenye daladala.

Akizungumza na waandishi katika Hoteli ya Ramada iliyopo Posta jijini Dar, Paul Makonda alisema kuwa ili kuendana na kasi ya rais hasa kwenye kuboresha sekta ya elimu nchini, alipata wazo la kuhakikisha wilaya yake inapambana ipasavyo na changamoto zinazowakabili walimu hasa suala la usafiri linalorudisha nyuma ufanisi wa walimu.

Makonda alisema kuwa suala hilo litazigusa pia Wilaya za Temeke na Ilala ambapo mwalimu atapatiwa kitambulisho maalumu chenye jina la shule, picha yake, saini ya mkuu wa wilaya na namba ya mwalimu mkuu.

Hata hivyo alisema kuwa usafiri huo utaanza rasmi Machi 7 mwaka huu ambapo walimu hawatatozwa nauli yoyote kuanzia saa 11:30 hadi saa 2:00 asubuhi na saa 9:00 hadi saa 12:00 jioni huku akitahadharisha kuwa ofa hiyo itakuwa endelevu kwa siku za kazi, yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa tu.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Daladala (Darcoboa), Sabri Mabrouk; Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji Abiria Dar (Uwadar), William Masanja na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva (Tadu), Shaban Mdemu walimpongeza Makonda kwa wazo hilo na kuwataka walimu washirikiane nao kufuata utaratibu huo huku wakiwataka wakuu wa wilaya kote nchini kuiga mfano huo katika wilaya zao.

Picha/Habari: Chande Abdallah/ GPL

Leave A Reply