The House of Favourite Newspapers

Walimu wakuu 90 shule za msingi, sekondari kuvuliwa vyeo kwa udanganyifu

0

1.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

2.Mkuu huyo akionesha msisitizo wa jambo wakati akifafanua hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa na wanahabari.Mkuu huyo akionyesha msisitizo wa jambo wakati akifafanua hoja mbalimbali zilizokuwa zimeulizwa na wanahabari.

3.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Salum Hapi, amesema kuwa walimu wakuu 68 wa shule za msingi na 22 shule za sekondari watavuliwa vyeo  kwa kosa la udanganyifu wa takwimu  za idadi za wanafunzi hewa tangu elimu itangazwe kuwa bure katika wilaya za Kinondoni na Ubungo.

Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake amemwagiza Katibu Mkuu Tawala wa Mkoa kuwavua walimu hao vyeo vyao na kuwapa walimu wengine kwa sababu ya kosa hilo.

Hapi alifafanua kuwa wakuu hao wamekuwa na wanafunzi hewa 2,534 kwa shule za msingi za wilaya ya Kinondoni.

Baadhi ya shule alizozitaja zilizo na wanafunzi hewa  ni Bunju B yenye wanafunzi 155, Goba Mpakani wanafunzi 42, Hananasifu 154 na Boko wanafunzi 74 huku shule za sekondari zikiwa ni Msisiri B wanafunzi 395, Ubungo Msewe 267 na Upendo 273 na nyinginezo.

NA DENIS MTIMA/GPL

MAJINA YA SHULE HIZO NA MAJINA YA WALIMU WAKUU kinondoni 2 (2)kinondoni 2 (1) kinondoni 3

MAJINA YA SHULE HIZO NA MAJINA YA WANAFUNZI HEWAubungo 2 ubungo 3 ubungo 4

ubungo 1

Leave A Reply