The House of Favourite Newspapers

Walinda Amani Umoja wa Mataifa Wafyatua Risasi na Kuua Raia Nchini Congo

0
Raia nchini Congo wameandamana kupinga uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Beni nchini humo

WATU wawili wameripotiwa kuuawa na wengine 15 kujeruhiwa baada ya wanachama wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwafyatulia risasi raia wanaopinga uwepo wa makundi hayo nchini humo.

 

Tukio hilo limetokea Jumapili katika mpaka wa mji wa Beni ambapo Brigedi ya majeshi ya MONUSCO yalikuwa yakiingia nchini Congo yakitokea katika nchi ya Uganda.

Askari wa Kulinda amani kutoka Umoja wa Mataifa wakifyatua risasi kuwatawanya raia

Video za tukio hilo ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha walinda amani hao wakifyatua risasi kwa raia kwa kile kilichosadikiwa kuwa ni raia kuwarushia mawe walinda amani hao.

 

“Katika tukiohilo askari kutoka Brigedi ya MONUSCO alifyatua risasi kwa raia pale mpakani pasipo kuwa na sababu ya msingi na kulazimisha kupita.” Taarifa iliyotolewa na Tume ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Kasindi nchini humo.

Umoja wa Mataifa umesema tayari mhusika ameshatiwa nguvuni kwa ajili ya uchunguzi

Muwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Congo Bintou Keita amesema uchunguzi umeshafanyika na tayari mtuhumiwa ameshakamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Leave A Reply