The House of Favourite Newspapers

Walioambukizwa Corona Uganda Wafikia 18

0

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amesema idadi ya maambukizi nchini humo imefikia 18 baada ya vipimo 197 vilivochukuliwa jana kuthibitisha kuwa watu wanne wameambukizwa COVID-19.

 

Wanne hao walikuwa karantini katika hoteli zilizoainishwa na serikali na wamepelekwa Hospitali ya Mulago kwa matibabu.

 

Aidha,  amesema wagonjwa 14 waliokuwa wamelazwa katika miji ya Entebbe, Masaka na Mulago wanaendelea vizuri.

 

Ameongeza kuwa mkakati wa kuwapima joto wasafiri viwanja vya ndege, kuwaweka karantini wanaoshukiwa kuwa na maambukizi na kuwatafuta wale ambao wamekuwa wakikimbia karantini umeonyesha matokeo mazuri.

Leave A Reply