Waliofariki Ajali Lori la Mafuta Morogoro Wafikia 68

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe amesema waliofariki dunia baada ya lori la mafuta kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta, wamefikia 68.

Dk Kebwe amesema awali waliofariki dunia walikuwa 62, lakini kati ya majeruhi 66 Sita wamefariki dunia na kuongeza idadi ya waliokufa.

Wakati mkuu huyo wa Mkoa akieleza hayo, kamishna a wa operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi, Lebaratus Sabas amewataka wananchi kuacha tabia ya kukimbilia kwenye maeneo ya hatari.


Amebainisha kuwa polisi walifanya msako maeneo ya jirani na ilipotokea ajali hiyo na kukamata madumu 15 ya mafuta ya dizeli yenye lita 260.

Amesema madumu hayo yaliibiwa na kufichwa katika mabanda ya jirani na ilipotokea ajali hiyo barabara ya Dar es Salaam-Morogoro mita 200 kutoka kituo cha mabasi cha Msamvu, kwamba chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.

RAIS MAGUFULI ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO/AMTUMA WAZIRI MKUU


Loading...

Toa comment