The House of Favourite Newspapers

Waliokufa kwa Corona Brazil Wafikia 400,000

0

IDADI  ya waliokufa kutokana na janga la virusi vya corona nchini Brazil imefikia watu 400,000 hadi jana katika wakati ambapo taifa hilo linapambana kupata chanjo za kutosha kudhibiti kuenea zaidi kwa kadhia hiyo.

 

Jana wizara ya afya ya nchini humo iliripoti vifo vya watu 3,001 ndani ya muda wa saa 24 na kufanya jumla ya watu waliokufa kufikia 401,186, idadi inayoifanya Brazil kuwa taifa la pili kwa idadi kubwa ya vifo vya Covid-19 nyuma ya Marekani.

 

Taifa hilo lenye uchumi mkubwa kwenye kanda ya Amerika ya Kusini limeshuhudia ongezeko la kutisha la maambukizi ya virusi vya corona tangu kuanza kwa mwaka 2021 huku hospitali karibu zote zikizidiwa kwa wingi wa wagonjwa.

 

Serikali ya nchi hiyo inahangaika kutafuta shehena ya dozi za chanjo ya Covid-19 baada ya kufanikiwa kutoa chanjo ya kwanza kwa raia milioni 28 pekee ambayo ni asilimia 13 ya watu wa taifa hilo.

Leave A Reply