The House of Favourite Newspapers

Waliomlawiti Mwanachuo na Kumdai Pesa Wafikishwa Kisutu

Mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, Anna Mwaisumo, 23,  (wa kwanza mbele kushoto) alipofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mtuhumiwa Samson Kisuguta (28) alipofikishwa Kisutu.

MFANYABIASHARA Samson Kisuguta (28) na mwanafunzi wa Chuo cha Ardhi, Anna Mwaisumo (23) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kumlawiti mwanachuo (jina limehifadhiwa kwa ajili ya maadili) na kushinikiza awape pesa.

 

Watuhumiwa hao wanaodaiwa kuwa wapenzi,  wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono,  mbele ya Hakimu Mkazi, Ally Salum,  ambapo wanadaiwa  walikula njama ya kulawiti na kujipatia fedha.

 

Kombakono amedai kuwa kosa la kulawiti  walilitenda Desemba 10, 2017 katika nyumba ya kulala wageni (jina limehifadhiwa) jijini Dar es Salaam ambapo walimlawiti mwanachuo mmoja.

 

Kosa jingine ni kusambaza picha za ngono, ambapo washtakiwa hao wanadaiwa Oktoba 7, 2018, maeneo ya jijini la Dar es Salaam walichapisha kupitia makundi ya WhatsApp picha za ngono za mwanachuo huyo huku wakijua ni kinyume na sheria.

 

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na kosa la kudai pesa ili wasisambaze picha za ngono, ambapo wanadaiwa walilitenda Novemba 13, 2018 wakiwa jijini Dar es Salaam ambapo walijipatia fedha taslimu Sh. 250,000 kutoka kwa mwanachuo huyo ili wasisambaze picha zake za ngono walizompiga.

 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, wakili Kombakono amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na washtakiwa hao walikana makosa hayo.

 

Mahakama iliwapatia washtakiwa masharti ya dhamana  ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya shilingi laki tano, lakini hawakuyatimiza.   Kesi imeahirishwa hadi Januari 3,  2019.

 

Comments are closed.