The House of Favourite Newspapers

Waliomuua RPC wa Mwanza Wahukumiwa Kunyongwa

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne kati ya saba waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza (RPC), Liberatus Barlow.

 

Hukumu hiyo imetolewa jijini Mwanza jana Jumanne Novemba 12, 2019 na Jaji Sirialus Matupa baada ya Mahakama kuridhika bila shaka yoyote na ushahidi uliowasilishwa na washtakiwa walitenda kosa hilo.

 

Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Muganyizi Michael, Magige Mwita, Abdallah Petro na Abdulrahaman Ismail.

 

Walioachiwa huru na Mahakama baada ya ushahidi kutowatia hatiani katika kesi hiyo ya mauaji namba 192/2014 ni Chacha Mwita, Buganizi Edward na Bhoke Marwa.

 

Kamanda Barlow aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio lililotokea eneo la Kitangiri Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza saa 8:00 usiku wa kuamkia Oktoba 13, 2012.

Comments are closed.