Walionaswa Vituo vya Masaji Watoa Ushuhuda Mzito!

 

Kwa waliobahatika kusoma gazeti la jana la Uwazi, watakuwa wanaelewa nini tumeamua kukichimba na kukianika kwa manufaa ya taifa letu. Wewe ambaye ndiyo kwanza unaanza kusoma makala haya iko hivi;

Kitengo cha Operesheni Fichua Maovu ‘OFM’ kwa muda mrefu kimekuwa kikifanya uchunguzi na sasa kimebaini uwepo wa utitiri wa vituo vya masaji ‘Massage Parlor’ katika miji mbalimbali ikiwemo Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya na kwingineko!

Wewe msomaji unaweza kuwa shahidi wa uwepo wa mabango kibao yanayotangaza huduma hiyo na ukawa unajiuliza kwamba, ni kweli Tanzania kuna uhitaji mkubwa wa vituo hivyo kiasi cha kutapakaa kila sehemu?

Na je, yanayofanyika ndani yake ni yapi? Ni huduma za masaji kama zilivyosajiliwa au kuna biashara nyingine haramu inayoendelea?

OFM imefanya uchunguzi wake na kubaini kwamba, kuna hatari kubwa inalinyemelea taifa endapo vituo hivi vya masaji vitaachwa vijiendeshe kinyume na taratibu na vingine kuendelea kusajiliwa bila kuwepo mipango madhubuti ya kuvidhibiti.

Ukijaribu kuchunguza utagundua kuwa, vitendo hivi vya ngono vinavyofanyika ndani ya baadhi ya vituo vya masaji, wanaohusika zaidi ni wahudumu na si wamiliki, licha ya kwamba kuna wamiliki wengine wanatajwa kunufaika na biashara hiyo.

KIVIPI?

Baadhi ya wahudumu ambao waliwahi kunaswa kwa nyakati tofauti wakifanya vitendo vya ngono kwenye vituo hivyo vya masaji waliweka bayana kuwa, wanalazimika kujihusisha na biashara hiyo kwa kuwa, hawalipwi mishahara.

“Sikatai, mimi najipatia pesa kwa njia hii, akija mteja akataka kafanyiwa masaji, anafuata taratibu za kiofisi lakini akishaingia chumbani na mimi, ni suala la kumshawishi kumpa huduma ya penzi kwa kulipia.

“Ni wachache sana wanaoishia kufanyiwa masaji ya kawaida tu kisha wakaondoka, wanaume wengi ni dhaifu kwa hiyo ukimfanyia ‘viuchokozichokozi’ tu mwenyewe anaomba msaada na hapo ndipo na sisi tunapojipatia pesa,” anasema binti aliyejitambulisha kwa jina la Sauda, aliyewahi kunaswa akifanya vitendo vya ngono kwenye kituo kimoja cha masaji kilichopo Sinza Mori jijini Dar.

MSIKIE NA HUYU;

“Mteja anapokuja unaweza kumwambia kuwa masaji ni kiasi fulani, labda ile ya mwili kwa mwili. Sasa mnapoingia huko chumbani na kuanza kufanya masaji, kwa kuwa mnakuwa wawili tu na hamna nguo, baadaye anageuka na kudai kuwa amezidiwa.

“Anakutaka mfanye mapenzi na anakuongezea pesa. Unakuta na wewe una shida zako, huwezi kuziacha pesa.

“Unakuta tunashawishika na kufanya mapenzi kwa sababu ya pesa. Mtu akikolea, anachukua mawasiliano yako na mara kwa mara anakuwa anakuja kwa ajili ya kupata huduma, wakati huu unakuta hataki masaji tena, bali ngono tu,” anasema Amina, mtoa huduma ya masaji kwenye nyumba moja iliyopo maeneo ya Mikocheni B jijini Dar.

OFM YABAINI FUSKA MKUBWA

Mmoja wa makamanda wa OFM hivi karibuni aliingia kwenye kituo kimoja cha masaji kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam na kukutana na mazingira ya kustaajabisha sana kama anavyotoa ushuhuda huu:

“Nilipoingia mle ndani, nilikutana na mandhari ya kuvutia sana, pale mapokezi kuna kama sebule hivi, walikuwepo mabinti wapatao 5, wote wakiwa wameumbika na nguo walizovaa, hazikuwa za heshima hata kidogo.

“Nilipojisogeza kwenye meza ya dada wa mapokezi kisha kuomba huduma ya masaji nikieleza kuwa, nasumbuliwa na maumivu ya mgongo, ghafla niliona wale mabinti wakianza kunigombea, kila mmoja alitaka kunifanyia.

“Kuna waliofikia hatua ya kuniita baby, honey na majina mengine kama hayo. Hata nilipomchagua mmoja wao kwa kumnyooshea kidole, nilipoingia naye kwenye kachumba nilianza kukutana na ushawishi wa hali ya juu.

“Haraka nilibaini pale siyo kituo cha masaji bali ni danguro. Hebu jiulize, wakati yule binti namkuta pale mapokezi alikuwa amevaa gauni flani hivi lakini alipokuja kunifanyia masaji alikuja akiwa amevaa kanga moja, hapo unatarajia nini?”

Sasa swali la kujiuliza ni je, nani wenye mamlaka ya kudhibiti hivi vituo vya masaji?

Hili tutakuja kulijadili kwenye Gazeti la Amani kesho! Usikose kwani kumbuka hatupoi mpaka kieleweke.

 Na Mwandishi Wetu, Risasi
Toa comment