The House of Favourite Newspapers

Waliotubu kwa DPP Kutorosha Kobe 201, Wahukumiwa – Video

WASHTAKIWA waliokuwa wakituhumiwa kutorosha kobe, wamehukumiwa kulipa fidia ya sh. milioni 40 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya uhujunu uchumi kwa kujihusisha na nyara za serikali bila kibali.

 

Watuhumiwa hao ambao ni David Mudi mkazi wa Ilala, Mohamed Salum Mohamed, Mustapha Bakari, Salum Wakili na Shabani Haji wote ni wakazi wa Zanzibar walikuwa wakituhumiwa kutorosha kobe 201 wenye thamani ya  sh. milioni 30 bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

 

Mbali na adhabu hiyo, washtakiwa hao wamepewa adhabu ya kifungo cha nje kwa sharti na kutofanya kosa hilo tena na washirikiane na serikali kutoa taarifa za watu wengine wanaojihusisha na makosa kama hayo.

 

Akitoa hukumu hiyo jana Jumanne, Oktoba 8, 2019, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Janet Mtega,  amesema  washtakiwa hao watalipa fidia hiyo ya sh. milioni 40 kwa utaratibu ulioonyeshwa katika hati ya makubaliano.

 

Washtakiwa hao ni miongoni mwa washtakiwa walioandikia barua kukiri na kuomba msamaha kwa Mkurugenzi wa Mashtaka  (DPP).

 

Katika kesi hiyo, washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kosa moja ambapo kati ya Novemba 1 hadi 16 mwaka 2015, kati ya maeneo ya Zanzibar na Dar es Salaam, wote walijihusisha na usafirishaji wa kobe 201 wenye thamani ya sh. milioni 30 milioni bila kibali kutoka mamlaka husika.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on

Comments are closed.