Walioua watu 14 Marekani nao wauawa

ndugu

Mmoja wa ndugu wa marehemu akifarijiwa.

Polisi katika Jimbo la California nchini Marekani wametaja majina ya washukiwa wawili ambao wameuawa kwa kuhusika na vifo vya watu 14 waliouawa kwa kupigwa risasi katika Mji wa San Bernadino jana.

Watu hao ambao ni mwanaume na mwanamke waitwao Syed Rizwan Farook, 28, na Tashfeen Malik, 27, wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi na polisi.

usa

Farook alikuwa ameajiriwa na baraza la mji kwa miaka mitano, mkuu wa polisi wa San Bernadino Jarrod Burguan ameeleza.

Shambulio hilo lilitokea jana wakati wa hafla katika ofisi moja. Maelezo kuhusu waliofariki bado hayajatolewa.

Tukio hilo ni baya zaidi katika matukio ya ufyatuaji wa risasi dhidi ya umma nchini Marekani tangu watu 26 wauawe katika shule moja mjini Newtown, Connecticut mwaka 2012.

_87005559_san_bernadino_shooting_v02_624map

Ramani inayoonyesha tukio lilipotokea.

Bw. Burguan, amesema watu 17 walijeruhiwa na kwamba polisi wana kila sababu ya kuamini kwamba wawili hao pekee ndio waliohusika kwenye shambulio hilo.

Shambulio lilo lilitekelezwa katika kituo cha Inland Regional Center ambacho huwasaidia walemavu na watu wenye matatizo ya kiakili. Hata hivyo, ufyatuaji risasi huo hauonekani kuwa na uhusiano na wagonjwa hao.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache tu baada ya watu watatu kuuawa katika kliniki ya Colorado Planned Parenthood.

Rais wa Marekani, Barack Obama ameshutumu shambulio hilo.

“Jambo moja tunalojua ni kwamba visa hivi vya ufyatuaji wa risasi humu nchini haviwezi kulinganishwa na kwingine duniani.”

Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kijasusi la FBI David Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi sasa haijafahamika.

“Kwa wakati huu ninaelewa moja ya maswali yenu ni kuhusu tukio hili la kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa hiyo tunaanzia mwanzo kufanya kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili.

Credit: BBC

Loading...

Toa comment