The House of Favourite Newspapers

Waliowapa Mimba Mastaa Hawa Ni Utata!

0
Hamisa Mobeto

 

UTATA na hali ya mkanganyiko inatawala miongoni mwa wadau kuhusiana na baadhi ya mastaa kuonekana kuwa na mimba, licha ya kutoweka wazi mahusiano yao, jambo ambalo linazua tafsiri tofauti ukilinganisha na nafasi zao kwa jamii.

WANAOTAJWA KUWA NA MIMBA

Ipo orodha ndefu ya mastaa wanaotajwa kuwa wajawazito, lakini wanaoonekana na kila dalili za mimba ni Video Queen Hamisa Mobeto, Muigizaji Skyner Ally na Husna Maulid.

Hawa ndiyo mastaa wenye muonekano wa ‘kimimbamimba’ lakini hawajaweka wazi wahusika, jambo linalowafanya baadhi ya mashabiki wao kubaki na sintofahamu ya nani wahusika.

Hamisa amewahi kujihusisha kimapenzi na mmoja wa wamiliki wa redio moja maarufu Bongo kisha wakaachana akiwa na mtoto mmoja lakini kuanzia hapo hakuwahi kuanika mwanaume aliyeuteka mtima wake hadi hivi karibuni ilipodaiwa kuwa ana ‘kibendi’.

 

Husna Maulid

 

Husna naye aliwahi kuwa kwenye uhusiano na Mkongo aliyefahamika kwa jina la Mwami Rajab, baadaye wakamwagana kabla na yeye hivi karibuni kuonekana na mimba kubwa tu.

Mwenyewe alipoulizwa kama mimba inamhusu nani alidai ni ya Mkongo licha ya baadhi ya watu wake wa karibu kudai kuwa, hapo kati alinasa kwenye penzi la mwanaume mwingine hivyo kuna utata wa mmiliki wa mimba hiyo.

Kwa upande wa Skyner, chanzo chetu kilidai kuwa tangu ajifungue mtoto aliyezaa na msanii Nay wa Mitego, amekuwa msiri sana kuweka wazi uhusiano wake ingawa kwa sasa kuna kila dalili za kuwa ni mjamzito ingawa mwandishi wetu alipomuuliza juu ya madai hayo aliwaka na kutaka aachwe na maisha yake.

KUNA HAWA WAWILI PIA

Ukiondoa wasanii hao, wapo Mwanamuziki Esterlina Sanga ‘Linah’ na Muigizaji Esha Buhet ambao wanatarajiwa kujifungua muda wowote kuanzia sasa, huku tofauti yao na orodha ya hapo juu ni kwamba wao wahusika wa mimba zao wanajulikana na wanaishi pamoja, huku Esha akiwa ameolewa.

Skyner Ally

 

KUTOKA DAWATI LA IJUMAA

Hakuna jambo jema maishani kama kupata mtoto. Ni furaha na zawadi pekee ambayo Mungu alimpa mwanadamu kama faraja toshelezi ya maisha. Lakini pamoja na hayo, zipo njia ambazo mtoto anapaswa kupatikana ikiwa ni pamoja na wahusika kuwa katika ndoa halali.

Ingawa pia, hata mtoto aliyepatikana nje ya muungano sahihi wa ndoa thamani yake ni ileile, lakini mshibo wa uhalisia hukamilika pale njia ya kwanza ikitumika.

Rai yetu kwa mastaa, wakiwa kama vioo vya jamii, siyo sahihi sana kupata mimba huku wakificha wahusika, jambo ambalo hutafsirika vibaya kwa jamii, kwani wao ni wa kuigwa na watu, ingawa pia kupata mimba na kuzaa nje ya ndoa si kosa kisheria- Mhariri.

NA WAANDISHI WETU | DAR

 

Msukama – Ni Bora Kuishia la Saba Kuliko Kuwa na Vyeti Halafu Huna Akili

Leave A Reply