The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Walisema Mwakyembe Hatohudhuria Kuapishwa! – Rais Magufuli

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 24, 2017 amewaaapisha; Jaji Stella Esther Mugasha kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Sylvester Mabumba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Job Masima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Israel, Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na sheria na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Lakini pia alikosoa taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari ikidai kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana angezungumza na waandishi wa habari leo wakati yeye amemtuma nchini India ambapo atakuwa huko kwa muda wa zaidi ya siku 10.

Pamoja na hayo amezungumzia upotoshwaji wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini.

“Namshukuru Waziri Dkt Mwakyembe amekuja hapa kuapa sababu jana kwenye mitandao kuna wengine walikuwa wakisema hatokuja kuapa, na nilikuwa nasubiri nione” alisema Rais Magufuli

NIMEKUWEKEA VIDEO USIKILIZE MWENYEWE HAPA

Comments are closed.