The House of Favourite Newspapers

Walter Chilambo Ampandisha Mpenzi Wake Stejini – Video

IKIWA ni mwendelezo wa vibe la Kongamano la Victory Campus Night la mwaka 2019, muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Walter Chilambo, usiku wa kuamkia leo amemtambulisha rasmi mpenzi wake (pichani) baada ya kupanda naye kwenye jukwaa kabla ya kutumbuiza katika tamasha hilo.

 

Katika kongamano hilo ambalo limefanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers usiku wa leo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu waliofika kwa ajili ya kumshukuru Mungu na kukutana na marafiki, Chilambo alianza kumtambulisha mpenzi wake huyo na kusema; “Naomba leo nimtambulishe rasmi mpenzi wangu, huyu mama ndiye ananifanya niwe hivi nilivyo, ninampenda sana.”

 

 

Chilambo na mpenzi wake (hakumtaja jina)  walishangiliwa na jukwaa mzima kisha akaanza kufanya shoo yake iliyowasisimua mashabiki wake na watu waliokuwepo viwanjani hapo.

 

Tamasha hilo lililoandaliwa na Kanisa la VCCT – Mbezi Beach, chini ya Mchungaji Dkt. Huruma Nkone limetikisa Jiji la Dar es Salaam licha ya mvua kunyesha lakini watu walijaa uwanjani na ratiba ikaenda kama ilivyokuwa imepangwa.

 

Katika tamasha hilo, ambalo lilianza majira ya saa 1:00 jioni, waimbaji mbalimbali walipanda jukwaani kuimba wakimsifu Mungu.  Baadhi yao ni, Upendo Nkone, AIC Chang’ombe Kwaya, Joel Lwaga, Walter Chilambo na wengine wengi.

PICHA NA: RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

 

Comments are closed.