The House of Favourite Newspapers

Wananchi Wanaomiliki Ardhi Mabwepande Waiangukia Serikali Inshu ya Uvamizi

0

WANANCHI wanaomiliki mashamba na viwanja eneo la Mabwepande wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameiomba serikali kuingilia kati kwa kuwaondoa watu waliovamia na kujimilikisha maeneo hayo kinyume cha sheria.

Ombi hilo limetolewa Julai 16, 2022 na wawakilishi wa wamiliki hao baada ya juhudi zao za kuwaondoa wavamizi kushindikana kwa vile wamekuwa wanapokea vitisho na baadhi yao tayari wamekatwa mapanga

 

Mmiliki mwingine Bw. Pascal Mbikilwa ambaye anamiliki eneo lenye ukubwa wa ekari 61 sehemu ya Kinondo Kata ya Mambwepande alisema kulikuwa na machimbo ya kokoto Nyakasangwe jirani na eneo hilo ambapo  watu hao wachimba kokoto walianza kuvamia na kukata viwanja na kuuza.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mji Mpya Kata ya Mabwepande, Bw. Mohammed Basta amekiri kuwepo kwa uvamizi huo lakini akashauri kwa vile maeneo mengi yameendelezwa kwa watu kujenga nyumba ni vema Serikali ikatafuta muafaka na wamiliki halali ili kuondoa mvutano uliopo.

 

Mwnanachi aliyenunu ardhi kutoka wka wavamizi na kuiendelezakwa kujenga nyumba Bi.Faiza Amour amesema yeye hakujua kama eneo hilo alilonunua na kujenga lilikuwa sio eneo halali la aliyemuuzia na kuiomba serikali iweke utaratibu wa kuwamilikisha kisheria maeneo hayo nay eye yuko tayari.

Leave A Reply