The House of Favourite Newspapers

Wamarekani, Wasauzi Kufunika Kampeni ya Castle Lite

0
Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa Kuwaunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe.

Dar es Salaam, Mei 20, 2017- Kampeni ya  “CastleLiteUnlocks” imetangaza  bahati nasibu zaidi kwa wiki kwa ajili ya wateja wake wa bia ya  Castle Lite Premium Lager ambapo washiriki watanunua tiketi kupitia TigoPesa.

Ili kushiriki  katika bahati nasibu hiyo mteja anachotakiwa  kufanya  ni kununua bia ya Castle Lite na kunakili namba zilizopo katika mfuniko wa chupa (kwenye ganda la plastiki) na kutuma namba hiyo kwa kutumia mfumo huu: *149*14#.

Akizungumza jana  kuhusu washindi,  Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wa  Kuwaunganisha Wateja Afrika Mashariki, George Kavishe,  alisema kila wiki jumla ya washindi 220 watajishindia  jumla ya shilingi 10,000 za muda wa maongezi. “Mbali na muda wa maongezi  zitakuwepo tiketi 30 za Watu Mashuhuri (VIPs) zitakazoshindaniwa ambapo washindi watatu watakuwa wanatangazwa kila wiki.

Pia alisema zitakuwepo tiketi 500 za kawaida ambapo watakuwa wanapatikana washindi 50  kila wiki kwa muda wa wiki kumi.

Kavishe pia alitangaza habari njema kwa wateja akisema sasa wanaweza kupata tiketi kwa ajili ya  kushiriki tamasha kubwa la CastelLiteUnlocks  kupitia huduma ya TigoPesa  kwa kutuma malipo yao kupitia  namba ya TigoPesa 0674-44-44-44.

Wateja wa mitandao mingine watanunua tiketi kwa kutuma namba hiyohiyo kupitia huduma ya kutuma ujumbe Kwenye Mitandao Mingine halafu wachague ‘Tigo Pesa’ katika simu zao.

“Bei ya tiketi ya kawaida ni  shilingi 20,000, lakini wateja watakaonunua kupitia TigoPesa  watafurahia punguzo la  shilingi 5,000 kwa kulipa shilingi 15,000 kwa tiketi moja,” aliongeza.

Kampeni ya CastleLiteUnlocks ni promosheni  inayoendeshwa na (TBL) ambayo lengo lake ni kuvutia soko kwa kuwazawadia wateja wa Castle Lite na  kuwashukuru kwa kuiamini na kuiunga mkono chapa hiyo. Kampeni hiyo itahitimishwa na tamasha kubwa la muziki  ambapo nyota wa muziki waalikwa watakuwa ni Future Gwiji wa Muziki wa Pop wa Marekani, Cassper Nyovest,  kutoka Afrika Kusini na wanamuziki wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Kavishe, bonanza kubwa la fainali  litafanyika Julai 22, katika viwanja maarufu vya Leaders, jijini Dar es Salaam.

HABARI: RICHARD BUKOS / GPL

Leave A Reply