Wambura amuandikia barua Karia

Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura.

AMEANZA kazi! Unaweza kusema hivyo kufuatia Makamu wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura, kumuandikia barua ya kiutendaji rais wa TFF, Wallance Karia.

 

Mwishoni mwa mwaka jana TFF ilikata rufaa katika Mahakama Kuu Tanzania Desemba 11 baada ya mahakama hiyo kutengua maamuzi ya Kamati ya Maadili ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni iliyomfungia Wambura kujihusisha na soka maisha, Machi mwaka jana kutokana na madai ya ubadhilifu wa fedha.

Rais wa TFF, Wallance Karia.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Wambura alisema kuwa, tangu aliporejeshwa na Mahakama Kuu anaendelea na shughuli zake za kiutendaji ndani ya TFF kama kawaida na kudai kuwa tayari ameshamuandikia barua Karia inayohusiana na kikao cha kamati ya utendaji na sasa anasubiria majibu.

 

“Naendelea na mchakato wangu, mimi nafanya kazi ninazopewa na rais japokuwa bado sijapewa kazi yoyote hadi sasa, pia kama kuna jambo ambalo nataka kumtaarifu naandika kupitia kwa katibu wangu.

 

“Hivi sasa kuna barua ambayo nimemwandikia rais wangu inayohusiana na masuala ya kiutendaji, hivyo nasubiria majibu nadhani hata waandishi mtaelezwa nini kinaendelea,” alisema Wambura.

Stori na Khadija Mngwai

Loading...

Toa comment