WAMBURA ASOMEWA MASHTAKA 17, KUTAKATISHA MKWANJA TSH. MIL 75

BAADA kukamatwa jana na kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, aliyekuwa Makamu wa Rais Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura amesomewa mashitaka 17 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo Februari 11, 2019.
Katika mashtaka hayo, Wambura anatuhumiwa kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha kiasi cha shilingi milioni 75 wakati akilitumikia Shirikisho hilo.
Kesi imeahirishwa hadi Februari 14, mwaka huu kwa ajili ya Hakimu kuamua kama aifute kesi ama la, Wambura amepelekwa rumande kusubiri uamuzi wa Mahakama.

Toa comment