The House of Favourite Newspapers

Wambura augua, akwama kufi ka mahakamani

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura

KESI inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura, jana Alhamisi ilishindwa kuendelea baada ya mtuhumiwa huyo kushindwa kutokea mahakamani kutokana na kuugua.

 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, Kelvin Mhina, jana alipokea taarifa kutoka magereza mbele ya mahakama hiyo iliyosemaWambura alishindwa kufi ka mahakamani hapo kutokana na kuwa mgonjwa.

 

Hata hivyo, wakili wa upande wa serikali, Ester Martin uliiambia mahakama kuwa kwa upande wao serikali wanaendelea na upelelezi wa kesi hiyo kama kawaida. Wambura anakabiliwa na mashitaka 17 likiwepo lile la utakatishaji wa fedha na kughushi nyaraka akiwa mfanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 9, mwaka huu.

Comments are closed.