The House of Favourite Newspapers

WAMEKUZA ‘VISU’ BILA WANAUME!

Image result for kajala na mtoto wake

WATU wengi huamini kwamba malezi bora ya watoto hutoka kwa wazazi wote wawili yaani baba na mama.

Mtoto anapolelewa na mzazi mmoja hususan wa kike, mara nyingi jamii imekuwa ikiamini kwamba ni rahisi sana kuharibikiwa kutokana labda kudekezwa na mzazi anayemlea au kukosa ile hofu ya mzazi wa pili hususani wa kiume.

 

Kwenye ulimwengu wa mastaa, wapo wasanii wa kike ambao pengine kutokana na jinsi wanavyoishi wao, wengi wamekuwa wakidhani labda watoto hao wa kike wangeweza kuharibika kimaadili lakini badala yake, wamesimama kidete kuhakikisha wanaishi katika misingi ya kimaadili.

 

Mastaa hao wamejitahidi kuwalea watoto wao wa kike warembo (visu) ambao umri wao tayari umekwenda kwenye ‘kuchangamka’ lakini hawajajiingiza kwenye mambo mabaya na wanawasomesha vizuri.

 

Mastaa hao ni pamoja na Kajala Masanja mwenye mtoto wa kike aitwaye Paula ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 16 na Yvonney Cherry ‘Monalisa’ aliyebahatika kumpata mtoto wa kike aitwaye Sonia (16).

Wengine ni Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye mtoto wake wa kike anaitwa Iptysam (14) na Chuchu Hans ambaye mtoto wake wa kike anaitwa Farhia (14).

 

Kimsingi hawa wote, Mungu amewajaalia kuzaa watoto warembo, lakini hawajawalea watoto hawa wakiwa na baba wa watoto hao.

Nini siri ya ushindi wao katika suala zima la maadili kwa watoto wao? Hivi ndivyo walivyozungumza mara baada ya kuzungumza na mwanahabari wetu kwa nyakati tofauti:

 

KAJALA

“Mimi ni mama halisi kabisa ninapokuwa nje ya nyumbani kwangu, na ni mama mkali sana kwa mwanangu Paula, ananijua vizuri kabisa kuwa mama hataki mchezo na mimi ninachotaka kwa mtoto wangu kuwa na heshima, kwa sababu anapoenda kinyume na mimi lazima nimpe adhabu ambayo inastahili.

 

Unajua mimi nimepitia changamoto nyingi katika malezi ya kulea mwanangu, nikiwa mwanamke tena mwenyewe bila baba, ningemlegezea ndio angeniletea shida sana lakini najua nikitetereka ndio ningemuharibu lakini nashukuru Mungu sasa anamaliza kidato cha nne. Nathubutu kusema; nimeweza na bado naendelea kukaza buti afike mbali.”Image result for monalisa na mtoto wake

MONALISA

“Unajua mtoto siku zote akikusumbua ujue mizizi yako haiko imara, mimi namshumkuru Mungu kanijalia mtoto wa nidhamu, mimi mwenyewe kama mama niko imara kumuangalia kwa kila kitu, japokuwa nimemlea mwenyewe kama mama kwa asilimia kubwa lakini nimejua kusimama imara na ninashukuru Mungu karibia anamaliza kidato cha nne sasa hivi.”

Image may contain: 2 people, people standing

NISHA

“Mimi ni msanii lakini linapokuja suala la malezi kwa mtoto wangu nakuwa mama na sio msanii tena. Kwa sababu ninajaribu sana kila wakati kuzungumza naye na kumuelimisha baya na zuri mpaka sasa nashukuru Mungu ni msikivu na ananielewa.”Image result for chuchu hans na watoto wake

CHUCHU

“Mimi najua wazi kazi yangu ni msanii lakini kamwe simshirikishi mtoto wangu katika vitu vyote vya kisanii, japokuwa anapenda na nilishawahi kufanya naye lakini katika kumlea ni lazima kabisa kumfundisha na ninavaa uhusika wa mama kabisa! Maana mtoto wa kike ni rafiki lakini pia usimuachie akakuzidi akili ni tatizo.”

Makala: Imelda Mtema

Comments are closed.