The House of Favourite Newspapers

Wami Ruvu Wakamilisha Ujenzi wa Birika la Kunyweshea Mifugo

0


Bodi ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanikisha ujenzi wa mradi wa kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Mnazi Mikinda Kata ya Ruvu Stesheni, Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariky Mmasy amesema birika hilo limegharimu shilingi milioni 72.

Amesema hadi sasa wamejenga mabirika 14 ikiwa ni mpango mkakati wa kuhakikisha wanawajengea mazingira rafiki wafugaji ili kutoingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji.

Akizindua mradi huo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon almaarufu Niki wa Pili amewataka wafugaji hao kuutunza miradi hiyo.

Amesema serikali inahakikisha inapunguza changamoto za migogoro ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye vyanzo vya maji au mashamba ya wakulima, hivyo mpango huo unaakisi mkakati wa Taifa wa TUTUNZANE .

Naye mmoja wa wafugaji katika kijiji hicho, Eliza Ole Sagati ameshukuru kwa kupatikana kwa birika hilo na kuiomba serikali kujenga katika vijiji vingine kupunguza changamoto ya muingiliano wa mifugo na mashamba.

Leave A Reply