Wamiliki wa Pool Table Waagizwa Kuzisajili

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imewataka wamiliki wote wa pool tables kuhakikisha zinasajiliwa na kupatiwa leseni.

 

GBT yenye jukumu la kusimamia uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini imesema kuwa Kifungu Namba 52 cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha ya mwaka 2003 pool table zote zinatakiwa kusajiliwa ili kuwezesha uendeshaji wa mchezo huo kihalali.

 

Taasisi hiyo imesema kuendesha mchezo huo bila usajili ni kinyume sha sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi agizo hilo.

 
Toa comment