Wana CCM Wote Kesho Tuungane na Dkt. Samia Kwenda Kupiga Kura-CPA Makalla
“Kampeni tulizozifanya katika siku zote 6 na mimi sijapumzika nimefanya kampeni katika majimbo nane ya Uchaguzi wa Jiji la Dar es salaam kwa taarifa tulizonazo na Mikutano ilivyokuwa inaendelea ni wazi kwamba CCM itashinda kwa kishindo.”
Niwaombe Wana CCM na Wananchi wote kesho tuungane na Mhe Rais Dkt Samia kwani ataongoza Mamilioni ya Watanzania kwenda kupiga kura na yeye atashiriki kupiga kura kwake Chamwino kwani Rais amekuwa mfano mzuri alianza kushiriki Kujiandikisha na kesho atashiriki kupiga kura na yeye kama Rais ametangaza kesho ni siku ya mapumziko hivyo tuamke asubuhi sana kwenda kupiga kura.
Katibu wa NEC-Itikadi Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Makalla ametoa kauli hiyo akizungumza kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Mkoani Morogoro Mikumi.
CPA Makalla akiongea na Wananchi ameendelea kusisitiza kwa Wana CCM kesho baada ya kupiga kura watu warudi nyumbani kupumzika kwani CCM inaamini kura zetu zitalindwa na mawakala tuliowateua hatuna sababu yeyote yakuwa na wasiwasi kwani wale mawakala watakuwepo pale kuwalikilisha Chama chetu Cha Mapinduzi na kwasababu tumeweka wakala kila Kituo cha Uchaguzi tusifuate wale wenzetu wanaoambiana kuwa makamanda tukimaliza kupiga kura tubaki vituoni huo ni ukorofi.