Wanafunzi 11 Wakamatwa kwa Kuchoma Moto Shule

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia wanafunzi 11 akiwemo msichana mmoja kwa tuhuma za kuchoma moto Shule ya Sekondari Geita mara tatu tofauti kuanzia Julai 5, Julai 6 na Julai 14 huku likidai chanzo cha kufanya hivyo ni upendeleo waliokuwa wanaupata wanafunzi wanaokaa bweni.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema uchunguzi umeonesha moto huo haukusababishwa na hitilafu ya umeme wala miundombinu chakavu ya shule hiyo, bali ulisababishwa na wanafunzi watukutu.

 

Aidha, Kamanda Mwaibambe ameeleza kwamba kutokana na utovu wa nidhamu wa wanafunzi hao wa kutwa shuleni hapo, bodi ya shule iliazimia kuwaondoa wanafunzi wa kutwa na kubaki na wanafunzi wa bweni pekee ndipo wanafunzi ho walipopanga njama za uchomaji wa shule hiyo.


Toa comment