The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Chuo Kikuu Tumaini Mbeya usajili wawaliza

0

Chuo Kikuu Tumaini Mbeya

Na Mwandishi Wetu, Uwazi

MBEYA: Kilio kimetawala katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Mbeya kutokana na wanafunzi 150 wanaosomea fani ya Afya ya Jamii na Unesi ngazi ya cheti kutojua hatima yao baada ya kubakiza miezi mitatu kufanya mitihani ya taifa bila kusajiliwa.

Wanafunzi hao waliliambia Uwazi kwamba kero yao kubwa inayowaliza ni kukosa usajili kwani walidai walianza masomo yao tangu Novemba mwaka jana na wanatarajia kumaliza masomo hayo Septemba mwaka huu na muda wa usajili umeshapita.

Akifafanua zaidi mwanafunzi aliyejitambulisha kwa jina la Neema Msimu alidai kuwa uongozi wa chuo hicho umekuwa ukiwahadaa kuwa wasiwe na hofu kwa kuwa wameshasajiliwa, lakini walipofuatilia waligundua kuwa hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyesajiliwa.

“Kwa sasa hatujui kama tutafanya mitihani yetu kwa sababu kiutaratibu hakuna mwanafunzi anayeruhusiwa kufanya mitihani bila kusajiliwa,” alidai mwanafunzi huyo huku akilengwalengwa na machozi

“Tupo wanafunzi wa fani ya afya ya jamii 135 na fani ya unesi 17 jumla 152, wote hatujasajiliwa licha ya kuwa hatudaiwi ada yoyote kama tulivyokuwa tumetakiwa na uongozi wa chuo,” alisema.

Alidai kuwa mwanzoni walithibitishiwa kuwa wamesajiliwa lakini kiongozi mmoja aliwaambia kwa siri kwamba usajili hawajafanyiwa na walipofuatilia serikalini wakabaini kuwa kweli hawajasajiliwa huku mwanafunzi mwingine, aliyejitambulisha kwa jina moja la Idrisa akisema wana wasiwasi kuwa hawatafanya mitihani na kupoteza ada zao bure.

Viongozi wa chuo hicho walipofuatwa na mwandishi wetu hali ilikuwa tofauti. Makamu Mkuu wa Chuo, Dk. Mangele Mrigo akiwa na viongozi wengine walikuwa katika majadiliano na baadhi ya wanafunzi hao lakini baada ya kuona waandishi wa habari, waliwafukuza, ndipo wanafunzi wakaanza kuwazomea baada ya kuonekana kutotaka kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari.

Hata hivyo, baadaye kiongozi huyo, Dk. Mrigo alionana na mwandishi wetu ofisini kwake na kukiri kuwa wanafunzi hao walikuwa hawajasajiliwa lakini akawatupia lawama kwa kuita vyombo vya habari.

“Taratibu za kusajili wanafunzi hao zinaendelea kwa ushirikiano na serikali,” alisema Dk. Mrigo huku nje ya ofisi yake wanachuo wakiimba “Tunataka, kusajiliwa, tunataka, kusajiliwa.” Mkuu wa Chuo, Dk. Gwamaka Mwankenja hakupatikana.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply