The House of Favourite Newspapers

SKENDO: OFM Wajifanya Wanafunzi, Waingia Madarasani USDM na Kusoma Siku Tatu Bila Kustukiwa! (+Video)

0

         udsm-10

Kamanda Namba 1 wa OFM (kushoto) akizungumza na mmoja wanafunzi halisi chuoni hapo bila kugundulika.

Dar es Salaam: HEBU soma hii nayo kisha utafakari inawezekana vipi?; Ni vigumu kuamini lakini OFM wamethibitisha:

udsm-2

Kamanda Namba 2 wa OFM akielekea darasani.

Moja ya taasisi za elimu ya juu nchini Tanzania zinazotegemewa kitaaluma na zenye heshima kubwa katika jamii kama Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), ambazo zilitegemewa kuwa mfano katika udhibiti wa mianya ya watu wasio na sifa kuingia na kusoma katika majengo yake, chuo hicho kimeingia katika skendo kubwa baada ya ‘wanafunzi feki’ watatu ambao siyo wanafunzi wala hawatambuliki kabisa, kuweza kuingia na kusoma katika madarasa matano tofauti ya chuoni hapo kwa muda wa siku tatu mfululizo, Risasi Jumamosi linathibitisha.

udsm-3

OFM (aliyezibwa uso) akifuatilia kipindi darasani akiwa na wanafunzi  halisi.

Hali hiyo ilitokea baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa, ulinzi na udhibiti wa watu katika taasisi hiyo kubwa zaidi ya kisomi nchini siyo wa kuridhisha na kwamba mtu yeyote anaweza kuingia eneo lolote la chuo hicho na kufanya chochote bila kuulizwa au kuzuiwa.

Taarifa hizo zilidai kuwa, licha ya ulinzi hafifu, pia udhibiti wa watu wasio wanafunzi kutumia majengo, walimu na vibwete vya chuo hicho ni sawa na hakuna, kwani mtu yeyote anaweza kuingia darasa lolote na kufanya chochote bila kuulizwa.

udsm-5

Makamanda wa OFM wakitoka darasani maeneo ya UDSM.

Inadaiwa kuwa, baadhi ya watu wasio wanafunzi wala wafanyakazi wa chuo, wamekuwa wakifika chuoni hapo na kujichanganya kwenye vipindi vya masomo mbalimbali kwa fani tofautitofauti bila kushtukiwa na wahadhiri au wakuu wa idara za chuo hicho.

Habari zaidi kutoka kwa vyanzo vya kuaminika zilidai kuwa, watu wanaosoma kwa mtindo huo, huweza kuendelea kupata elimu hadi akazoeleka na pengine huja kushtukiwa unapofika wakati wa mitihani.

udsm-9

Makamanda wa OFM wakiwa katika majadiliano ndani ya eneo la chuo.

Baada ya kupata maelezo hayo ya awali, Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kiliamua kujipanga na kwenda kujiridhisha kama kweli udhaifu huo upo katika chuo hicho ambacho kimetoa viongozi mbalimbali wa ngazi ya kitaifa na kimataifa

udsm-6

Wanafunzi halisi wakijadiliana masomo darasani.

SIKU YA KWANZA OFM ‘MLIMANI’

kwa kupita mbele ya walinzi na hata kujichanganya kwenye vimbwete (mabenchi maalum yanayotumiwa na wanachuo kwa ajili ya kujisomea).

udsm-8

Makamana wa OFM na wanafunzi wengine wakifuatilia kipindi darasani.

Baadaye, vijana hao maalum kwa ajili ya habari za uchunguzi, waliingia katika madarasa matatu tofauti, wakianzia na darasa lililo katika Jengo la Sayansi ya Jamii, ambako hata hivyo, licha ya wanafunzi kuwepo na kushindwa kuwatambua, hadi saa moja baadaye walipoondoka, hakuna mwalimu aliyeingia darasani.

Baada ya kutoka katika darasa hilo, wakiwa hawana ‘beji’ kama wanavyuo wengine, waliliendea Jengo la Elimu ya Biashara, ambako waliingia madarasa mawili tofauti kwa muda wa zaidi ya nusu saa na kuondoka bila kutambulika.

udsm-7

Makamanda wa OFM wakifuatilia kipindi darasani.

SIKU YA PILI OFM CHUO KIKUU

Januari 7, mwaka huu, OFM waliingia tena mzigoni na safari hii walianzia katika Jengo la Elimu ya Biashara na kuzama kwenye darasa lililo chumba cha kwanza upande wa kushoto ambako bahati nzuri, walimkuta mwalimu akiendelea na somo liitwalo Marketing Network, ambako wote watatu waliingia na kuendelea na kipindi kama kawaida hadi kilipomalizika.

SIKU YA TATU…

udsm-1

…Wakiwa katika vimbwete wakifanya majadiliano na wanafunzi wa chuoni hapo.

Kufuatia kujiridhisha huko kuwa umakini ni sifuri na kwamba uwezekano wa watu wenye nia mbaya kufanya uchunguzi kabla ya kutekeleza lengo lao ni mkubwa, Risasi Jumamosi liliwasiliana na Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Profesa Florens Luoga na kumwelezea kuhusu udhaifu huo, ili kupata maoni yake.udsm-4

Kamanda Namba 3 wa OFM akizungumza na mmoja wa wanafunzi.

“Suala la uwepo wa wanafunzi hewa kuhudhuria vipindi madarasani haliwezekani, kila mwanafunzi aliyepo amesajiliwa na ana kitambulisho shingoni mwake, inawezekana kuwepo kwa kesi hiyo, lakini mimi bado sijaisikia.

“Hata hivyo, nitoe wito kwa wanafunzi wenye tabia hizo na niwasihi tu waache, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na siyo ungwana,” alisema Luoga.

MAHARIRI: Hingii akilini kuona mtu asiyekuwa mwanafunzi wala mtumishi wa chuo anaweza kuingia, siyo tu eneo la chuo, bali hadi darasani bila kugundulika kuwa si muhusika, hivyo hii ni changamoto kwa uongozi wa chuo ambayo wanatakiwa kuifanyia kazi. Lazima uwepo utaratibu na udhibiti ambao utawabaini haraka wageni na wanafunzi feki chuoni hapo!

Leave A Reply