The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Msingi na Sekondari Wapewa Mafunzo ya TEHAMA

0

 

 

Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi chache ambazo wanafunzi wake wa shule za msingi na sekondari wamefaidika na ujuzi na maarifa ya Tehama yaliyotolewa na kampuni ya teknolojia na usafirishaji ya inDrive ili kuwajengea uwezo wa kubuni njia bora za kutatua changamoto za usafirishaji nchini.

 

Mafunzo hayo ya siku moja yalitolewa kwa watoto wa makundi maalum na BeginIT, mradi wa kimataifa wa elimu ulioanzishwa na inDrive mwaka 2012 ili kuamsha shauku ya watoto kujifunza, ukuaji  binafsi na kushawishi uchaguzi wa mzuri wa taaluma ya baadaye.

Wanafunzi 39 kutoka shule tatu za msingi za Kinondoni, Msisiri na Mkuti na Shule moja ya Sekondari ya Debribant waliletwa pamoja katika Shule Kuu ya Habari na Teknolojia ya Mawasiliano ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kujifunza namna wanavyoweza kuitumia na kufaidika na mstakabali wa teknolojia ya mjongeo duniani (the future of mobility).

Pia mafunzo hayo yaliyokuwa yakitolewa na wataalam wa Tehama yalilenga kuwaandaa wanafunzi hao na mstakabali wao na kuwapa ushauri wa kitaalam kuhusu teknolojia mpya katika sekta ya elimu ambazo zinaweza kuboresha maisha yao na jamii inayowazunguka.

Tanzania miongoni mwa nchi chache duniani

Ndani ya mwaka 2022,  mradi huo ulilenga kuvifaidisha kimaarifa vituo 127 vya watoto yatima, makazi, na shule za vijijini katika chini 15 za Urusi, Kazakhstan, Brazili, Mexico, Colombia, Ecuador, Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Nigeria, Peru, Chile, Indonesia, India na Pakistan.

Wakati wa mafunzo hayo, wanafunzi walipata fursa ya kujadili, kuwasilisha mawazo na kazi zao bunifu zinazotoa suluhu za kiteknolojia kukidhi mahitaji ya jamii katika sekta ya usafirishaji.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Tehama ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mhandishi Eliud Kataraihya aliwaeleza wanafunzi hao kuwa zamani watu walilazimika kusubiri au kutafuta taxi mitaani ili kuwapeleka wanakotaka lakini kwa sasa kila kitu kinafanywa kutumia simu yako.

“Ukiwa na inDrive unaamua au mnaafikiana nauli, kipengele hiki ni cha kipekee kwenye soko.  Unapoona vitu vinabadilika kwa uzuri, hii ina maana kuwa kuna watu wako nyuma wanaofanya kazi kwa bidii kuleta suluhu,” amesema Mhandisi Kataraihya.

Leave A Reply