Wanafunzi wa DIT, CBE Waomba Ujenzi Eneo la Kuingia Lango Kuu la Chuo Kukamilika Haraka
Wanafunzi wanaosoma katika Chuo Cha Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi Kuu ya Dar es salaam wamemuomba mkandarasi anayejenga barabara ya Bibi Titi kuharakisha ujenzi wa kipande Cha eneo la Chuo Chao kutokana na maji ya mvua kutuama kwa muda mrefu katika lango kuu la kuingia chuoni kwao hali inayopelekea wao kupata adha kubwa namna ya kuingia na kutoka.
Wakizungumza na mtandao huu wamesema kuwa” hii si kwetu tuu hata wanaopita eneo hili imekuwa tabu tupu, hivyo tunaomba mamlaka husika zifanye haraka kujaza kifusi wakati ujenzi ukiendelea wa kuweka lami” walisikika wakieleza.