The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi wa Enaboishu kuanzisha umoja

1.Kutoka kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Zawadi Msalla, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Renald Shirima na mdau wa jumuiya hiyo, George Robert Nsonde.Kutoka kushoto ni Afisa Habari Mwandamizi wa Idara ya Habari (Maelezo), Zawadi Msalla, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Renald Shirima na mdau wa jumuiya hiyo, George Robert Msonde.

2.Shirima (Kulia) akisoma taarifa yake.Shirima (kulia) akisoma taarifa yake.
4Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

WANAFUNZI waliowahi kusoma kwenye shule ya Sekondari ya Enaboishu Mkoani Arusha wanatarajia kuanzisha umoja utakaojulikana kama ‘Enaboishu Sekondari School Alumni Association’.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa muda wa umoja huo, Renalda Peter Shirima, alipokuwa akizungumza na wanahabari kuwa umoja huo utalenga kusaidi masuala ya kitaaluma shuleni hapo kwa kuhamasisha wanafunzi kusoma kwa bidii na serikali kuinua elimu.

Shirima amesema lengo la umoja huo ni kuwakutanisha wahitimu wote waliosoma shule hiyo ili kusaidiana, kuchangia michango mbalimbali ya kuendeleza elimu shuleni hapo na kuweka mkakati wa kuishauri serikali namna bora ya kuwatumia wahitimu wa zamani wa shule mbalimbali nchini kuboresha miundombinu ya shule zilizopo nchini.

Alifafanua kuwa mkutano huo utafanyika kwenye matawi mawili ya Dar es Salaam, ambapo utafanyika kwenye viwanya vya Triple Seven Kawe wakati Arusha utafanyika kwenye viwanja vya AICC Club Kijenge Mogorofani. Mikutano hiyo itaanza Desemba 5.

(NA DENIS MTIMA/GPL)

Comments are closed.