The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi wa Marekani Watembelea Ofisi za Global Group

Wageni hao wakiwasili katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori.

 

WANAFUNZI kutoka Chuo Kikuu cha Case Western Reserve University cha Marekani mapema leo wamepata fursa ya kutembelea makao makuu ya ofisi za Global Group na kujionea namna kampuni hiyo inavyojiendesha katika shughuli zake mbalimbali za kihabari.

Viongozi wa Global Group wakiwapokea wageni hao.

 

Wanafunzi hao wakiwa kwenye picha ya pamoja ndani ya chumba cha mapokezi katika na baadhi ya wafanyakazi wa Global Group.

 

…Wakisoma baadhi ya magazeti yanayotolewa na Global Group.

Ugeni huo ulioambatana na kiongozi wao, Michael Goldberg ambaye ni mhadhiri katika chuo hicho, umepokelewa na Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho na Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Salehe Ally, ambapo kwa pamoja waliwatembeza katika ofisi zote zilizopo katika jengo hilo na kupata fursa ya kuwaeleza mambo machache ya kiutendaji.

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally akiwaelezea jambo wanafunzi hao.

Lengo la ziara yao, ni kutaka kujua jinsi wajasiriamali wa Tanzania wanavyofanya shughuli zao, changamoto wanazokumbana nazo na pia kutoa misaada kwa wale wenye biashara endelevu, zinazosaidia kutatua changamoto za jamii inayowazunguka.

Wakipandisha ngazi kuelekea News Room.

 

Mhariri Mtendaji, Saleh Ally (kulia), akisalimiana na mmoja wa wanafunzi hao wakati wakiwasili.
Wakipata maelezo zaidi katika ya ofisi ya Meneja Mkuu.

 

…Wakiwa katika chumba cha wasanifu kurasa wa magazeti.

 

…Wakiwa katika pichaya pamoja kwenye chumba cha Studio za Global TV Online.

 

PICHA: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL

Comments are closed.