The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi Wafaidika na Elimu ya Kuweka Akiba Kupitia Benki ya NMB

Wanafunzi wakipata elimu kutoka kwa Ofisa wa benki ya NMB, Monica Job (kulia).

 

Katika kutambua umuhimu wa vijana ambao ni Taifa la kesho, Wanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya
Wasichana ya Barbro Johansson Model iliyopo jijini Dar es Salaam, wamepata elimu ya fedha na umuhimu wa
matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki, walipotembelea Makao Makuu ya benki hiyo kujionea
shughuli mbalimbali za kibenki kwa vitendo.

Wanafunzi wakifurahi pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna na Mwalimu wao, Jennifer
Dominick.

 

Wanafunzi hao walipata nafasi ya kujifunza na kutembelea idara na vitengo tofauti ili kufahamu shughuli zao lakini
pia walitembelea Tawi la NMB Ohio.

Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna akikata keki pamoja na wanafunzi.
Kaimu Mkurugenzi wa NMB, Ruth Zaipuna (kulia) akilishwa keki na mmoja wa wanafunzi.

Pamoja na hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amewaasa wanafunzi hao kuwekeza nguvu
zaidi katika elimu, kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

…Wanafunzi wakipata elimu mbalimbali kuhusiana na elimu ya fedha na umuhimu wa
matumizi makini ya fedha ikiwemo kuweka akiba benki.

Baada ya mafunzo hayo, wanafunzi wote walipata nafasi ya kufungua akaunti zitakazowawezesha kutunza fedha
na kujijengea tabia ya kuweka akiba na kunufaika na huduma na bidhaa za benki ya NMB hususan Chipukizi na
Mwanachuo Akaunti.

 

 

Comments are closed.