TAASISI isiyo ya kiserikali ya HDIECA inayojishughulisha na mazingira, leo imewaongoza wanafunzi wa Sekondari ya Mashujaa jijini Dar es Salaam kupanda miti na maua katika maeneo ya shule hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Sarah Pima, amesema lengo la kuwashirikisha wanafunzi hao katika zoezi hilo ni kuwalea vijana katika hali ya kutunza mazingira.
Katika tukio hilo, taasisi hiyo ilikuwa na taasisi ya Jielimishe Kwanza na Aspect ambapo iliwafundisha wanafunzi hao mbinu mbalimbali za utunzaji wa mazingira na kujilinda na madhara yanayotokana na mazingira hatarishi kama vile kuvuta hewa isiyofaa na mengineyo.
Comments are closed.