Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Vyuo vya Afya vya Serikali 2020/21

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini.

 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) waliratibu udahili wa waombaji wa Mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Dirisha la udahili lilifunguliwa tarehe 15 Juni, 2020 na kufungwa rasmi tarehe 15 Agosti, 2020.

 

Jumla ya nafasi za udahili 3,586 katika vyuo vya umma vya Afya na Sayansi Shirikishi kwa kozi za Astashahada ya Msingi, Astashahada na Stashahada zilitangazwa. Kufuatia mchakato mzima wa udahili na uchaguzi imebainika kwamba walioomba na kuwa na sifa za kuwawezesha kujiunga na Mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2020/2021 walikuwa 14,074.

 

Idadi ya waombaji waliochaguliwa katika programu za Astashahada na Stashahada ni 3, 354. Idadi ya waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kwa kukosa nafasi ni 10,720.

 

Hivyo, Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji na umma kwa ujumla kwamba matokeo ya uchaguzi yametoka rasmi leo tarehe 3 Septemba, 2020 na yanapatikana akaunti (profiles) za waombaji na tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).

 

Baraza linawashauri waombaji ambao hawakuchaguliwa kutuma maombi kwenye vyuo vingine vinavyoendelea kufanya udahili hadi tarehe 15 Septemba, 2020 dirisha la udahili litakapofungwa.

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

3 Septemba, 2020

 

TAZAMA ==> JINA LAKO HAPA

Toa comment