The House of Favourite Newspapers
gunners X

Wanafunzi Waliopata Ujauzito Kurejeshwa Shuleni ni Uamuzi wa Serikali

0

Rais Samia, ametoa ufafanuzi kuhusu kauli iliyotolewa siku za hivi karibuni na Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako inayowahusu wanafunzi wote walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro na mimba kuwa watarejeshwa rasmi shuleni.

Rais Samia amesema kuwa uamuzi huo ni uamuzi wa Serikali na kuwa watoto wote walioacha shule kwa sababu ya utoro, utukutu, mimba sasa watawezza kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa shule ya msigi ya Museveni iliyopo Chato mkoani Geita, unaofanywa na Rais Museveni, mapema Novemba 28, 2021.

“Tumeamua watoto wote walioacha shule kwa utoro, utukutu, mimba warejee darasani tunawapa nafasi nyingine ya kuweza kusoma tena” Amesema Rais Samia.

Aidha amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo kwani elimu ni haki ya msingi kwa kila mtanzania hivyo hawaoni sababu za kuwabana wanafunzi hao ambao wapo tayari kuendelea na masomo.

Ameongeza kusema kuwa Serikali imejipanga vyema katika kufanikisha suala hilo kwa kuanzisha ‘Elimu Mbadala’ ambayo itatumika endapo mwanafunzi atachagua kusoma nje ya mazingira ya awali.

“Ni suala la kujipanga, wale ambao wanahisi kuwa hawataweza kurejea tena shule tumewawekea ‘Elimu Mbadala’ (Alternative Education) watakwenda kwa mkondo huo, tuwafundishe namna ya kujiingiza kwenye miradi wajitafte kwa manufaa yao na watoto” Amesema Rais Samia.

Amewatoa shaka wale wote wenye hofu juu ya maadili ya wanafunzi ambao wapo mashuleni kufuatia ujio huo wa walioacha shule kuwa Serikali ipo makini katika kutekeleza mpango huo.

“Kuna waliofurahia na kuna waliochukia juu ya hili, nimeona nilitolee ufafanuzi kwa maana tayari limeaanza kuzua mijadala huko, tupo makini na sula hili na niwahakikishia kuwa halitaathiri wengine” Ameongeza kusema Kiongozi huyo Mkuu wa Nchi.

Leave A Reply