Wanafunzi Wanaodaiwa Kuua Waruhusiwa Kujiandaa na Mtihani

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Katoro Islamic wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanafunzi mwenzao, Mudy Muswadiku, wameruhusiwa kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne wakiwa gerezani.

Mahakama imetoa ruhusa hiyo baada ya Mwalimu Majaliwa Abdu ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa kuomba wanafunzi hao waruhusiwe kuwa na madaftari yao ili waendelee kujiandaa na mitihani itakayoanza Novemba 4, 2019.

Wanafunzi hao wametakiwa kuwasiliana na mamlaka ya Magereza ili waletewe madaftari, vitabu na kalamu na waendelee kujisomea.

Wanafunzi wanaoshtakiwa ni Sharifu Huled (19), Abdallah Juma (19), Hussein Mussa (20), Sharifu Amri (19), Fahadi Abdulaziz Kamaga (20) na mlinzi wa shule, Badru Issa Tibagililwa (27).


Loading...

Toa comment