The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi wapongeza ofa punguzo la ada

0

mlimani

Wanafunzi wa Chuo cha  cha Mlimani School of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam.

WANAFUNZI mbalimbali wanaojitokeza kujiunga na Chuo cha Mlimani School of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam, kinachotoa ofa ya punguzo la ada wamepongeza hatua hiyo.

Wakizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, wanafunzi hao walisema mpango maalum wa kuwasomesha kwa ada nafuu uliofanywa na chuo hicho umefufua upya matumaini yao ya kupata elimu na hatimaye ajira.

MLIMANI“Nimemaliza Kidato cha Nne mwaka 2010, sikuweza kuendelea na masomo kwa sababu ya kukosa ada, nashukuru chuo hiki kimeweka punguzo kubwa ambalo wazazi wangu sasa wanamudu kulipa, nimefurahi,” alisema John Peter mkazi wa Sinza, Dar.

Naye Jane Nkumba anayetarajia kuanza masomo yake ya Uandishi wa Habari katika chuo hicho kupitia mpango huo alisema: “Nina kipaji cha utangazaji, nilikuwa sina pa kuanzia lakini sasa ndoto yangu itatimia.”

Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani, Hassan Ngoma (pichani) amewapongeza wazazi wanaojitokeza kutumia fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huo ni endelevu kwa sababu umelenga kuwakomboa vijana kielimu.

“Hatutaacha kuisaidia jamii yetu, tunaendelea kutoa taaluma katika masomo ya Business Admistration, Banking and Finance, Accountancy, Human Resource Management, Procurement and Supply, Journalism and Mass Communication na Information Technology,” alisema Ngoma anayepatikana kwa simu namba 0715-200900.

Leave A Reply