The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi wawili Walijiteka na Kuomba Fedha Kwa Wazazi, Tunawashikilia

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawashikilia wanafunzi wawili kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na watekaji na kuomba pesa kutoka kwa familia zao.

Akizungumza leo Februari 04, 2024, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema Januari 26, 2025 baada ya kutolewa taarifa za kupotea kwa mabinti hao Jeshi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwapata na kisha kuwahoji kwa kina juu ya tukio hilo wasichana hao wawili ambao ni mwanafunzi wa Kidato cha Pili (16) na mwingine Mwanafunzi wa Darasa la saba (12) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es salaam.

Kamanda muliro alisema wasichana hao wanashikiliwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira ambayo yanaonyeshe kuwa wametekwa na watekaji wanataka pesa.

“Katika uchunguzi wetu na ufuatiliaji ulifaonywa na jeshi la polisi mara baada ya mahojiano ya kina na watoto hao ambao walikiri kutengeneza tukio hilo la uongo ili waweze kujipatia pesa kwa udanganyifu toka kwa wazazi wao” Alisema Kamanda Muliro.

Alisema mara baada ya kutoweka Januari 26, 2025 na kuelekea Longoni Beach ambapo walikesha hapo hadi Januari 27 asubuhi na baadae kuelekea maeneo ya Tungi mpaka walipokamatwa wakizunguka.

“Jeshi linalaani na kukemea vikali vitendo hivyo vya watu kujiteka kwa lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu na kusisizita kuwa jeshi halitasita kuwachukua hatua kali wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo”. Alisema kamanda Muliro