The House of Favourite Newspapers

Wanafunzi wazidi kumiminika baada ya ofa ya punguzo la ada

0

mlimaniNa Mwandishi Wetu

WANAFUNZI mbalimbali wamezidi kumiminika kujiunga na Chuo cha Mlimani School of Professional Studies cha jijini Dar es Salaam, kinachotoa ofa ya punguzo la ada kwa wanafunzi hao.

MLIMANIAkizungumza na gazeti hili, mkurugenzi wa chuo hicho, Hassan Ngoma alisema tangu watoe ofa hiyo ya punguzo la ada wamekuwa wakipokea wanafunzi wengi kila siku jambo linalomfanya awapongeze wazazi na walezi wanaojitokeza kupeleka vijana wao kutumia fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huo ni endelevu kwa sababu umelenga kuwakomboa vijana kielimu.

“Hivi sasa muamko wa wanafunzi kujiunga na chuo unazidi kuwa mkubwa, ninamatumaini baada muda mchache nchini kutakuwa na wataaluma wazuri katika masomo ya Business Adminstration, Banking and Finance, Accountancy, Human Resource Management, Procurement and Supply, Journalism and Mass Communication na Information Technology,” alisema Ngoma.

Kwa upande wao, baadhi ya wanafunzi waliobahatika kujiunga na chuo hicho wamezidi kuupongeza mpango huo maalum wa kuwasomesha kwa ada nafuu uliofanywa na chuo hicho na kuongeza kuwa kwa kiasi kikubwa umefufua upya matumaini yao ya kupata elimu ikiwa ni hatua moja kwenda kupata ajira.

“Vijana tunaotoka katika mazingira ya familia za kimaskini tumekuwa tukikabiliwa na changamoto kubwa ya kupata ada, kwa hiyo fursa hii iliyopatikana ya kupunguziwa ada, kwa kiasi kikubwa itawasaidia wanafunzi wengi,” alisema Mary Andrew aliyejiunga hivi karibuni chuoni hapo.

Mbali na wanafunzi waliozungumza na gazeti hili, pia kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wamekimwagia sifa kemkem chuo hicho wakidai ni mkombozi wa maisha ya baadaye ya watoto wao kwenye suala zima la elimu.

“Kijana wangu anapenda sana kuwa mwandishi wa habari ila nilishindwa kumsomesha kutokana na kuwa sina kipato cha kueleweka, lakini kupitia mpango huo maalum nimemuandikisha kuanza masomo ili atimize ndoto yake,” alisema Ismail Mohammed mkazi wa Tandale kwa Mtogole.

Nafasi za kujiunga na chuo hicho bado zinapatikana, kwa yeyote anayehitaji kujiunga amtafute mkurugenzi wa chuo hicho kupitia namba ya simu 0715-200900.

Leave A Reply