The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi Waiga Staili ya Makambo

STRAIKA wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo, amewaambukiza aina ya ushangiliaji wake timu ya Wanawake ya JKT Queens, ambapo wamekuwa wakishangilia kwa staili yake kila wanapopachika bao.

 

JKT watumia aina hiyo ya ushangiliaji Juzi Jumatano katika mchezo wao dhidi ya Simba Queens wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara, ‘Serengeti Lite Premier League’, uliopigwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Gazeti hili liliwashuhudia wachezaji wote wa JKT Queens, timu ambayo inamilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa, wakishangilia kwa staili hiyo mara baada ya kupata bao lao la kuongoza, jambo lililozua mshangao mkubwa kwa baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba waliokuwepo katika kushuhudia mchezo huo uliokuwa wa kasi na upinzani mkubwa kutoka kwa timu zote mbili.

Comments are closed.