The House of Favourite Newspapers

Wanajeshi Watano wa Marekani Wafariki Dunia Baada ya Helikopta Kuanguka

0

Wanajeshi watano wa Jeshi la Marekani, wamefariki dunia baada ya helikopta waliyokuwa wakiitumia kwenye mafunzo ya kijeshi, kuanguka Mashariki mwa Bahari ya Mediterania.

Kamanda wa Jeshi la Marekani barani Ulaya, amenukuliwa akisema wanajeshi wote watano kwenye ndege hiyo, walifariki baada ya hitilafu kutokea wakati wakijaza mafuta angani kama sehemu ya mafunzo ya kijeshi.

Taarifa za awali za ajali hiyo, zilitangazwa Jumamosi na maelezo kamili yakatolewa Jumapili huku jeshi hilo likieleza kwamba juhudi za kutafuta miili ya waliofariki, zilianza mara moja kwa kushirikisha vikosi vya ndege na meli za kijeshi za Marekani zilizopo karibu.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin alisema kwenye taarifa yake kwamba: “Tunalia kwa huzuni kubwa kwa kifo cha kusikitisha cha watumishi watano wa Marekani wakati wa ajali ya mafunzo katika Bahari ya Mediterranean mapema Jumamosi.”

“Wakati tunaendelea kukusanya habari zaidi kuhusu ajali hii ya kusikitisha, hili ni funzo kwamba wanaume na wanawake jasiri wanaolinda taifa letu kubwa wanaweka maisha yao hatarini kila siku ili kuilinda nchi yetu,” alisema.

Leave A Reply