Wanajiolojia kuchunguza ardhi iliyopasuka na kumeza magari 12 Mississippi
Ardhi ilivyopasuka .
Meridian
WATAALAMU wa Jiolojia wameitwa kuchunguza ni jinsi ambavyo ardhi ilipasuka, kutitia na kumeza magari 12 katika maegesho ya magari kwenye mgahawa wa IHOP uliopo eneo la Meridian karibu na barabara Kuu ya Alabama jijini Mississippi nchini Marekani.
Tukio hyilo lililotokea juzi Jumamosi lilisababisha shimo kubwa lenye urefu wa futi 400 sawa na mita 120 na upana wa futi 35 sawa na mita 11 katika neneo la mgahawa huo huku jumla ya magari 12 yakimweza na shimo hilo.
Mwanzoni taarifa zilitolewa kuwa chanzo cha kutitia kwa eneo hilo ni kutokana na mvua kubwa kunyesha mfulurizo kwa wiki mbili eneo hilo na kusababisha hali hilo iliyopelekea ardhi kupasuka na kutitia, Lakini serikali ya Jiji la Mississippi imeamua kuita wataalam wa Jiolojia watakaoanza kazi leo kuchunguza kiundani tabia ya nchi ya eneo hilo na kilichopelekea mpaka ardhi kutitia na kusababisha madhara hayo.
Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho, na wahandisi wanatarajiwa kudadisi uthabiti wa ardhi eneo hilo leo.