Wanakijitonyama Dar hapa ni usafi Tu!
WAKAZI wa eneo la Kijitonyama Mpakani ‘A’ jijini Dar es Salaam, wamefanya usafi leo katika mitaa inayozunguka maeneo yao hadi mpakani mwa Sinza Afrika Sana huku wakisema kauli mbiu yao ni ‘Hapa ni Usafi Tu’.
Zoezi hilo ni muendelezo wa kauli ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwataka wananchi kufanya usafi kwenye maeneo yao ili kuweza kuondokana na ugonjwa wa kipindupindu kabla ya siku ya maadhimisho ya Sikukuu ya Uhuru, Desemba 9 ambapo mwaka huu itakuwa ni siku ya kufanya usafi.
NA DENIS MTIMA/GPL