The House of Favourite Newspapers

Wanamuziki wa Dansi wafurika kumzika Kasongo Mpinda

1Wanamuziki wa zamani wa Muziki wa Dansi waliofika kwenye msiba wa Kasongo Mpinda ‘Clayton’. Kutoka kushoto ni King Kiki, Shaban Scotto, Mkulu Wambagoi, Father Lusonz na John Ponteloks
2Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa akiwa pamoja na baadhi ya wanamuziki wa dansi.
3Mwanamuziki wa Dansi, Kassim Mapili akitoa salamu kwa waombolezaji kwa niaba ya wanamuziki wote wa Dansi.
4Waombolezaji waliobeba mwili wa marehemu wakielekea makaburini, Kisutu kwa ajili ya mazishi.IMG_0006

Mwili wa marehemu ukizikwa.

IMG_0009

IMG_0013

Umati wa watu ukimzika marehemu Kasongo Mpinda ‘Clayton’.

WANAMUZIKI wa zamani wa muziki wa Dansi nchini, mchana wa leo wamemiminika kwenye msiba wa mwanamuziki mwenzao, Abubakari Kasongo Mpinda ‘Clayton’, aliyefariki dunia jana jioni nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa maradhi ya Kisukari.

Baadhi ya wanamuziki hao waliofika kwenye msiba kwa ajili ya kushiriki mazishi yaliyofanyikia kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar ni John Peter Pontelokis, Father Lusonz, Mkulu Wabangoi, Shaban Scotto, Kassim Mapili na King Kiki.

Mbali na wanamuziki hao, walikuwemo pia wasanii kutoka tasnia mbalimbali pamoja na Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa.

Marehemu Clayton alizaliwa February 2, 1945 katika mji wa Lubumbashi Jimbo la Shaba. Alifika Tanzania mwaka 1979 akitokea Jamhuri ya Kidemokrasia Congo (DRC), ameacha mke na watoto wanne.

Enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi katika bendi nyingi nchini zikiwemo Marquis Du Zaire, Mk Group na Bana Marquis.

(PICHA, STORI: GABRIEL NG’OSHA NA BONIPHACE NGUMIJE/GPL)

Comments are closed.