Wananchi Buchosa wampongeza Mbunge Eric Shigongo kwa Elimu ya Ujasiliamali
Elimu ya ujasiliamali iliyotolewa na mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kwa wananchi wa Buchosa imekuwa mkombozi kwako baada ya wananchi hao kutumia elimu hiyo kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinafanya kuendesha maisha yao.
Kauli hii imekuja siku chache baada ya Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kutoa kiasi cha Sh500,000 kwa kikundi cha akina mama wa CCM kata ya Nyehunge walioamua kuunda umoja wao baada ya kupata mafunzo bure kupitia ofisi ya Mbunge wa Buchosa.
Katibu wa umoja wa akina mama Kata ya Nyehunge (UWT) Kalunde Masanja amesema akina mama Kata Nyehunge wanamshukuru Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kwa kuwapatia mafunzo bure ambayo yamewasaidia kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinawasaidia kuendesha maisha yao.
Sambamba na kuendelea kuwasaidia fedha za kuongeza mtaji ambao itawasaidia kukuza biashara zao na kujiinua kiuchumi.
“Tunamshukuru Eric Shigongo kwa kuwajali akina mama Buchosa kutoa mafunzo bure ya ujasiliamali sambamba na kuendelea kuwawezesha fedha za kuongeza mtaji wao tunaadi tutaendelea kukuunga mkono kutokana na jitihada anazozifanya Kwa wananchi wake , amesema Masanja.
Didas Gaitan lunyungu mwalimu bingwa wa ujasiriamali na mkurugenzi wa kampuni ya mjasiriamali kwanza enterprises amesema ofisi ya Mbunge wa Buchosa iliona jambo la kwanza Kwa wanabuchosa nikutoa mafunzo bure ya ujasiliamali ili wananchi wake wapate uelewa wa kutengeneza vitu mbalimbali kwa ajili ya kujikwamua na wimbi la umaskini.
“Leo matunda ya mafunzo yetu ya ujasiliamali tunayaona akina mama wanafahamu kutengeneza mambo mablimbali ,vikiwemo Sabuni, mafuta nk tutaendelea kutoa mafunzo zaidi ili Buchosa tuwe na viwanda vidogo vidogo, amesema Lunyungu.
Baadhi ya wananchi wamepongeza jitihada zinazofanywa na mbunge wa Buchosa Eric Shigongo za kuwaletea wananchi wake maendeleo ili wajitegemee kiuchumi .Hivyo tunatakiwa kukuunga mkono aendeleo kuwatumikia wananchi wa Buchosa Ili wapate maendeleo.