The House of Favourite Newspapers

Wananchi Dozi Tu

0

TIMU ya Yanga ambao wanajiita ‘Wananchi’ imeendeleza wimbi la ushindi baada ya leo kuvunja mwiko wa kuifunga Biashara United ya Musoma kwenye dimba lake la nyumbani kwa goli 1-0 mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Karume mkoani Mara bao pekee likikwamishwa wavuni na mshambuliaji Michael Sarpong dakika ya 68 ya mchezo baada ya kupokea pasi kali kutoka kwa Ditram Nchimi ‘Duma’.

 

Biashara walikuwa na rekodi nzuri mbele ya Yanga hasa wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, ambapo hawajafungwa kwa miaka mitatu, lakini leo Yanga walionekana dhahiri kushinda kwani muda mwingi walikuwa wakilisakama lango la Biashara ambao wameendelea kubaki nafsi ya nne wakiwa pointi 16.

 

Baada ya mechi ya leo Yanga imesalia nafasi ya pili mwa msimamo wa Ligi hiyo kwa kufikisha pointi 22, sawa na Azam Fc ambao wamecheza mchezo mmoja zaidi ya Timu ya wananchi, mechi inayofuata ni dhidi ya Mnyama Novemba 7.

Leave A Reply