Wananchi:  Kinondoni sisi ni Idd azzan tu

IDD AZZAN (2)Na Mwandishi Wetu

Wananchi wa Jimbo la Kinondoni wameeleza jinsi walivyo na imani kubwa na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Idd Azzan anayetetea nafasi yake kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wakizungumza na waandishi wetu kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni inayoendelea sehemu mbalimbali za jimbo hilo, wananchi wengi walieleza kuridhishwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa kipindi chote tangu mbunge huyo alipoingia madarakani.

“Mbunge wetu siyo longolongo kama wanasiasa wengine, yeye akiahidi kitu lazima atekeleze, ndiyo maana hatuoni sababu ya kumchagua mtu mwingine Kinondoni, kiukweli Azzan anatosha, CCM mbele kwa mbele,” Masumbuko Laurent, mkazi wa Hananasif, Kinondoni aliliambia gazeti hili kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo uliofanyika siku chache zilizopita kwenye eneo hilo.

Naye Hamza Mwalyego, mkazi wa Kinondoni B, alisema yeye si shabiki wa CCM lakini kutokana na maendeleo ya haraka yanayoletwa na mbunge huyo, haoni sababu ya kutomuunga mkono.

“Unajua mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mimi nipo upinzani lakini sioni mtu wa kupambana na Azzan, mheshimiwa anafaa, anajituma na yupo karibu na wananchi, natamani wabunge wote wangekuwa hivi,” alisema.

Loading...

Toa comment